Tuzo za Kili Music Awards zilifanyika jana na msanii 20% aliibuka kidedea kwa kubeba jumlaya tuzo 5. Kusema ukweli kwangu mimi ilikuwa mara ya kwanza kulisikia hilo jina, kwahiyo nikaamua nitafute nyimbo zake. Kumbe ni msanii wa siku nyingi na nyimbo zake nilikuwa nshawahi kuzisikia ila basi tu jina halikunikaa kichwani. Kuna nyimbo moja hasahasa ambayo ulinikuna sana, inaitwa Maisha ya bongo, fungua boneti uicheki hapo chini....Hizi si nyimbo zilizompatia tunzo hizo tano, ila ni nyimbo ambazo mimi binafsi nimezipenda, hasahasa ujumbe wake...
Tuzo alizoshinda ni kama ifuatavyo;
- Wimbo bora wa Afro-pop
- Mtunzi bora wa nyimbo
- Mwimbaji bora wa kiume
- Wimbo bora wa mwaka
- Msanii bora wa mziki wa kiume
Hongera sana 20%.
Kuna wimbo wake mmoja ambao kaka yangu alikuwa anaupenda sana, na mpaka leo nikiusikia unanikumbusha kaka yangu huyo mpendwa, ucheki hapo chini
No comments:
Post a Comment