Swahili-vibes ingependa kutoa ombi kwa serikali ya Jamhuri ya Tanzania
kuweka mikakati dhabiti ambayo itahakikisha janga kama hili halitotokea tena katika jiji letu la Dar-es -salaam. Si siri kwamba hii si mara ya kwanza kwa mabomu kulipuka na wakti umefika kusitisha upotezaji wa maisha kwa hali hii ambyo inaweza kuzuilika kabisa. Blogu nyingi sana zimeongelea janga hili na watu wengi sana wametoa maoni yao, mambo ya uwajibikaji, utata katika majibu ya serikali n.k yameshaguswa, kwa hiyo sitosema mengi.
Pia, ningependa kusema kwamba nimefurahishwa sana kwa jinsi wanajamii wanavyotoa misaada kadri ya uwezo wao na umoja ulivyonyweshwa na watanzania katika kuhamasishana kuwasaidia ndugu zetu walioathirika. Hongereni sana.

No comments:
Post a Comment