Tuesday 22 February 2011

Kulipuka kwa mabomu Gongo Lamboto!!

Ningekuwa mtovu wa nidhamu kama ningewacha tukio kubwa kama hili lipite bila kutamka lolote.  Kwanza ningependa kutoa pole kwa wadau wote walioathirika na kulipuka kwa mabomu hayo huko Gongolamboto.  Mwenyezi Mungu awapunguzie mitihani na awape nguvu, uvumilivu na faraja katika wakati huu mgumu.

Swahili-vibes ingependa kutoa ombi kwa serikali ya Jamhuri ya Tanzania
kuweka mikakati dhabiti ambayo itahakikisha janga kama hili halitotokea tena katika jiji letu la Dar-es -salaam.  Si siri kwamba hii si mara ya kwanza kwa mabomu kulipuka na wakti umefika kusitisha upotezaji wa maisha kwa hali hii ambyo inaweza kuzuilika kabisa.  Blogu nyingi sana zimeongelea janga hili na watu wengi sana wametoa maoni yao,  mambo ya uwajibikaji, utata katika majibu ya serikali n.k yameshaguswa, kwa hiyo sitosema mengi.

Pia, ningependa kusema kwamba nimefurahishwa sana kwa jinsi wanajamii wanavyotoa misaada kadri ya uwezo wao na umoja ulivyonyweshwa na watanzania katika kuhamasishana kuwasaidia ndugu zetu walioathirika.  Hongereni sana.










No comments: